Robo Mwezi
Watumishi wa Campoverde
Imetafsiriwa na Kennedy Langat
Hakimiliki © 2019 M.G. Gullo M. Longo
Picha ya jalada na michoro iliundwa na kuahiririwa na Massimo Longo
Haki zote zimehifadhiwa
JEDWALI YA YALIYOMO
Sura ya KwanzaAnaepuka nikijaribu kumkumbatia...Sura ya KwanzaAnaepuka nikijaribu kumkumbatia...Sura ya PiliMnong'ono wa baridi ulikuwa ukimsumbuaSura ya PiliMnong'ono wa baridi ulikuwa ukimsumbuaSura ya TatuAligundua kuwa mvulana huyo alikuwa ametishika, na akaangua kichekoSura ya TatuAligundua kuwa mvulana huyo alikuwa ametishika, na akaangua kichekoSura ya TatuAligundua kuwa mvulana huyo alikuwa ametishika, na akaangua kichekoSura ya nneSauti ilikuwa ikinong'oneza masikioni mwake maneno kwa lugha isiyojulikanaSura ya nneSauti ilikuwa ikinong'oneza masikioni mwake maneno kwa lugha isiyojulikanaSura ya TanoAnakabiliwa na kitu cha kuogofyaSura ya TanoAnakabiliwa na kitu cha kuogofyaSura ya SitaHakuweza kutoa matamshi hayo kutoka kwa kichwa chakeSura ya SitaHakuweza kutoa matamshi hayo kutoka kwa kichwa chakeSura ya SabaWahusika wasioeleweka waliwashwa na sauti ya kutulizaSura ya SabaWahusika wasioeleweka waliwashwa na sauti ya kutulizaSura ya SabaWahusika wasioeleweka waliwashwa na sauti ya kutulizaSura ya NaneTafakari ya picha hiyo mbayaSura ya NaneTafakari ya picha hiyo mbayaSura ya TisaNgazi isiyo na mwishoSura ya TisaNgazi isiyo na mwishoSura ya KumiAlihisi kama angeweza kutoboa mbingu kwa mikono yake waziSura ya KumiAlihisi kama angeweza kutoboa mbingu kwa mikono yake waziSura ya Kumi na MojaWazo hili liliendelea kuitesa royo yakeSura ya Kumi na MojaWazo hili liliendelea kuitesa royo yakeSura ya Kumi na MbiliIlimkumbusha kinywaji cha vitunguu vya kiberitiSura ya Kumi na MbiliIlimkumbusha kinywaji cha vitunguu vya kiberitiSura ya Kumi na TatuAlishuka kutoka angani akikokota mawingu yake meusiSura ya Kumi na TatuAlishuka kutoka angani akikokota mawingu yake meusiSura ya Kumi na Nne Alishuka chini ya winguSura ya Kumi na Nne Alishuka chini ya wingu Sura ya Kumi na TanoKama kwamba alimezwa na DuniaSura ya Kumi na TanoKama kwamba alimezwa na DuniaSura ya Kumi na SitaGhafula kelele za ajabu zilisikika kama za kigugumizi cha kinaSura ya Kumi na SitaGhafula kelele za ajabu zilisikika kama za kigugumizi cha kinaSura ya Kumi na SabaAlikuwa akitembea vizuri wakati alipovuka kizingitiSura ya Kumi na SabaAlikuwa akitembea vizuri wakati alipovuka kizingitiSura ya Kumi na NaneMakucha yaliingia ndani ya ngozi yakeSura ya Kumi na NaneMakucha yaliingia ndani ya ngozi yakeSura ya Kumi na TisaKama kana kwamba ilikuwa Sukari ya barafu kupamba keki ya sifongo ya VictoriaSura ya Kumi na TisaKama kana kwamba ilikuwa Sukari ya barafu kupamba keki ya sifongo ya VictoriaSura ya IshiriniKila wakati mtoto akiniita kwa jina fulani, ndivyo nitakavyoitwaSura ya IshiriniKila wakati mtoto akiniita kwa jina fulani, ndivyo nitakavyoitwaDibaji
Dibaji
"Kila kitu kitakuwa sawa, wewe ni mvulana mkubwa sasa....Rudi na ucheze na Watoto wengine. Tutakutana tena, ninakuahidi''
Mtoto alimtazama akitiririkwa na machozi alipoondoka mtu ambaye amekuwa akicheza naye tangu mwanzoni.
Mtoto alikimbia kurejea kwenye vijigari kwenye bustani iliyojuani, ambako alikwenda kucheza na watoto wengine jirani, huku fikra za rafiki ya kimawazo zikififia polepole.
Baada ya kujipenyeza kwenye mahali watoto wengine walikuwa, hatimaye angeweza kupanda kwa kitelezo. Hakupoteza hata muda na alianza kuteleza kwenda chini ya kitelezo, akisukuma kwa bidii kadri awezavyo. Hakuteleza hata hadi mwisho, wakati alipoona msichana mwenye nywele nyeupe akikimbia kutoka kwa mama yake na kuelekea kwenye miguu yake. Hakuweza kupunguza mwendo na alimgonga kwa nguvu.
Msichana huyo mdogo alipoteza mwelekeo na kugonga kichwa chake kwenye ukingo wa kitelezo.
Alijaribu kumfikia mtoto huyo msichana ili kuhakikisha kuwa alikuwa sawa, lakini akasukumwa kando bila huruma na mamaye, ambaye alikuja kumwokoa. Ghafula, kundi la babu na akina mama walikusanyika karibu na msichana huyo maskini.
Alipokuwa akijaribu kutambaa mbali na miguu ya watu wazima, alihisi kwamba alikuwa amezimia. Mtu mmoja aliita ambulensi! Huku sauti hiyo ikijitokeza kwa nguvu kwenye maskio yake, alianza kuingiwa na hofu. Alikimbia kuelekea msituni nyuma ya bustani.
Ghafula, kila kitu karibu naye kikawa giza. Upepo baridi ulikuwa umesheheni sauti za kutisha. Mistari asiyoijua ilianza kuchanganyika na mazungumzo ya wazazi kwenye bustani. Zilikuwa zikitoka nyuma ya kundi la miti, ambayo vivuli vyao virefu vilikuwa vinajidhihirisha. Kisha, sauti hiyo ambayo ilikuwa ikijitokeza kutoka pande tofauti ilizidi kuendelea kusikika. Alikuwa akimfikia zaidi na zaidi, hadi alipohisi kuwa ilikuwa ikinong'oneza maskioni mwake:
"Damnabilis ies iom, mirdo cavus mirdo, cessa verunt ies iom, mirdo oblivio ement, mors damnabils ies iom, ospes araneus ies iom"
Aliweka kichwa chake kwenye mikono yake ili kutuliza sauti hiyo, lakini haikusaidia. Alipiga magoti na akafunga macho yake...
"Damnabilis ies iom, mirdo cavus mirdo, cessa verunt ies iom, mirdo oblivio ement, mors damnabils ies iom, ospes araneus ies iom"
Sura ya kwanza
Anaepuka nikijaribu kumkumbatia.
"Elio, Elio, njoo hapa! Nisaidie kuanua mboga kabla ya dharuba kuja, tafadhali."
Elio alikuwa amesimama wima akiwa amevalia viatu vyake vipya na alikuwa akimtazama mamaye, ambaye alikuwa akihangaika katika shughuli zake.
"Elio! Usisimame tu hapo! Chukua hii!" Alimtikisa na kuweka begi iliyojaa mboga kwenye mikono yake. Elio hakuwa na nia ya kufanya kitu kingine. Alipanda ngazi zilizoko nje ya jengo, akageuka na kufungua mlango. Alianza kutazama taa nyekundu ya lifti ambayo mwangaza wake haivumiliki. Kisha, akaacha kusubiri na kupanda ngazi kwenda kwenye nyumba yake gorofani. Aliweka mboga kwenye meza ya jikoni na kwenda moja kwa moja hadi chumba chake cha kulala kusikiza muziki kitandani.
Mara tu alipopanda gorofani mamake akaenda kumtafuta. Alisimama mlangoni akipiga kelele: Unafanya nini? Hatujamaliza bado, njoo unisaidie!".
"Sawa, nko njiani..." akajibu Elio bila kusonga. Kwa kweli alitaka tu kumwepuka. Giulia akatoka, akitarajia kwamba mara hii itakuwa tofauti. Hakuwa na matumaini. Alikuwa akihangaika kumtia moyo mwanawe, ambaye alikuwa akizidi kuwa mwenye kutojali. Kutoka Mlangoni, aliweza kusikia wazi hatua za dadaye huku akimwita kwa sauti ya furaha. "Elio! Elio! Ondoa makalio kitandani na uje usaidie mama. Anakusubiri huko chini." Alimfokea huku akifahamu kwamba itakuwa bure tu. Elio hakusonga hata inchi moja. Badala yake, aliongeza sauti ya muziki na kuendelea kutazama dari, kana kwamba hakuna kinachotendeka. Giulia, ambaye alikuwa amechoka kutokana na mabishano na mwanawe kuliko kutokana na uchovu, mwishowe alilazimika kupandisha mboga akisaidiana na bintiye, Gaia. Huku akipanda ngazi ya jengo hilo lililo na orofa tano, ambako lifti yaonekana kutofanya kazi kila siku (na kwa kejeli, siku sote haifanyi kazi wakati anapotaka kubeba mboga kupanda ngazi kwenda juu), aliendelea kufikiria kuhusu Elio. Jengo hilo lilipakwa rangi nyeupe na ya machungwa, kama majengo mengine ya baraza la Gialingua, mtaa ambao walikuwa wanaishi. Familia ishirini ziliishi katika mtaa huo, na zilikuwa zimegawanywa katika gorofa ishirini zilizoangalia pande tofauti ya jengo lenyewe.
"Hii ni mara ya mwisho unafanya hivi!" akamfokea akiwa jikoni. "Tutatatua hii punde to baba yako atakaporejea nyumbani!"
Elio hakuwa hata anamsikiliza kwa kuwa alikuwa amezama katika muziki huo wa kuchukiza. Hakuna na hakuna anayeweza kutikisa hisia za uchoshi na ubishi aliousheheni. Dunia yake isiyopendeza ilikuwa kama makazi kwake. Huo ndio ulikuwa utu wake na dunia ililazimika kumzoea. Gaia alikuwa tofauti kabisa: alikuwa na umri wa miaka kumi na mitano, ana macho angavu na nywele fupi nyeusi. Saa ishirini na nne hazikotosha kwake kushughulikia maslahi yake yote.
Giulia alikuwa mwanamke mwenye nguvu pia. Lakini, kinyume cha bintiye, alikuwa na nywele nyeupe zilizopindika, alikuwa mnene kiasi lakini mwepesi na aliyejitolea. Alikuwa mama wa kawaida mwenye umri wa miaka 42: kila wakati alikuwa na ratiba ngumu akijaribu kudumisha usawa kati ya kazi na familia.
Ilikuwa chakula cha jioni. Hata hivyo, hakuna kelele zilizosikika kutoka chumba cha kulala cha Elio. Kwa kweli, hajasonga tangu alipokimbia kujitosa kitandani na kuvaa vipokea sauti vinavyobanwa kichwani.
Alisikia sauti ya ufunguo katika kufuli wa mlango wa mbele. Wakati uo huo, huku mlango ukiwa bado haujafungwa vizuri, sauti ya hamaki ya Giulia tayari ilikuwa imemkera mumewe:
"Hatuwezi kuendelea kufanya hivi!"
"Mpenzi, wacha niingie chumbani kwanza..."
Giulia alimbusu mumewe na kurudi kulalamika.
"Ni kumhusu Elio, sivyo?" alisikika kama aliyekata tamaa wakati alipouliza.
"Ndio, ni yeye." akajibu Giulia.
Wakati uo huo, Carlo akatoa mkebe wa chakula ndani ya begi lake ambalo alikuwa akienda kuacha jikoni. Kisha, alikuwa akienda kuweka mkoba wake kwenye kabati la nguo. Ndani ya mkoba huo, kila wakati angeweka jezi ya ziada kwa kwa sababu ya mawimbi ya joto ambayo yalikuwa yakipiga eneo hilo mwezi huo wa Mei.
Alikuwa mwema, mwenye umri wa miaka arobaini na mbili, mrefu na mwembamba. Nywele zake zilikuwa zimegeuka kijivu, lakini wakati mmoja zilikuwa zinafanana na za bintiye. Uso wake uliochongoka ulikuwa wazi: kwenye pua lake lililofanana na mdomo wa ndege alikuwa akivalia miwani duara ya chuma.
"Tuizungumzie kumhusu baadaye?" kwa upole alimmwuliza bibiye, akitarajia kwamba atasononeka.
"Ndio, uko sahihi mpenzi." alijubu, lakini aliendelea kulalamika hadi wakati chakula cha jioni kilipoandaliwa.
Kwa bahati, Gaia hakuacha kuongea kuhusu siku yake, akichukulia machungu yake madogo kwa njia ya kutia moyo.
Giulia alikuwa amemaliza kuandaa mezani wakati aliposema:
"Umwite Elio."
" Haina maana na unaifahamu." alijibu. "Unajua hatasonga hata inchi moja, isipokuwa aitwe na baba..."
Giulia, kisha akamgeukia mumewe:
"Ameshinda katika chumba hicho tangu nilipomrudisha nyumbani kutoka shule. Anazidi kuwa mbaya."
"Si tulisema atakuwa akirudi nyumbani mwenyewe kuanzia sasa na kuendelea?"
"Nilikuwa katika eneo hilo...
Nilikuwa nikinunua mboga..."
"Kila siku unatoa vizingizio ili kumlinda, lakini tena unalalamika kuhusu tabia yake!"
Carlo alikuwa akitikisa kichwa chake kama ishara ya kutokubali. Kisha, akaamka kwenye kochi na kwenda kwenye chumba cha watoto.